Urembo wa Nywele

Habari mpendwa,

Leo tujifunze jinsi ya kukuza Nywele haraka na zenye afya kwa njia rahisi Sana kwa vitu vya asili,pia ni kwa Nywele fupi,ndefu, nywele zilizo dumaa na nywele zenye dawa.

Kuna njia nyingi Sana za kufanya Nywele zako zistawi kwa haraka na zijae.

1.Juisi ya kitunguu maji ;

Njia hii nzuri kabisa na isiyo na gharama.Kitunguu maji kina madini ya sulphur yaliyo na uwezo wa kubusti kuondoa collagen production( protini ngumu isiyoyeyuka na iliyoumbwa kama nyuzinyuzi )mwenye seli na kusaidia ukuzaji nzuri wa nywele Ila harufu yake isikufanye uiache kwa sababu ina matokeo mazuri sana.

Jinsi ya kuandaa

Katakata kitunguu chako vipande vidogovidogo na visage kwa kutumia Brenda .Kisha paka na sugua kwa ncha za vidole vyako Hadi kufika mwisho wa nywele na kuzimasaji vyema kuhakikisha kichwa chote imeenea,Kisha ziache kwa dakika 15, kisha zioshe kwa kutumia shampuu na maji Safi.

2.Tui la nazi na limao

Kwa kawaida tui la nazi lina madini ya chuma,patassium, na fat .

Jinsi ya kuandaa

Chukua nazi yako moja tu ikune vizuri ,weka maji ya vuguvugu kamua chuja weka mwenye chombo kisafi.Kisha chukua nusu kipande cha limao kamua maji yake,Kisha weka vijiko vinne mwenye tui lako la nazi ,Kisha weka vijiko vinne vya olive oil kisha koroga vizuri,Kisha paka mwenye nywele zako hakikisha unaweka ya kutosha na usugue kwa ncha ya vidole.

3.Maji ya Mchele

Maji ya Michele yana faida nyingi mwenye ngozi na nywele ila kwa hapa nazungumzia nywele tu ,ngozi nitaeleza kazi yake kipindi kinachofuata hapo baadae.

Husaidia;

– Kulainisha na kung’arisha nywele.

– Kuondoa muwasho na mba kichwani.

– Kujaza nywele kwa sababu yana amino acid.

Jinsi ya kuandaa

Andaa Michele 1/4 kilo, Osha vizuri Kisha weka mwenye sufuria safi,ongeza maji Safi,Kisha weka jikoni ufunike kwa dk10 na usiive Sana maana unatakiwa uwr kama unaelekea kulainika tu hivi,Kisha epua na uache upoe, Kisha chuja na weka mwenye kopo,Kisha funika kwa usiku mzima,asubuhi ongeza maji kikombe kimoja ili kupunguza nguvu,Kisha paka nywele zako maji zioshe na shampuu baada ya hapo zimwagie hayo maji ya Michele,Kisha vaa kofia ya nailoni kwa kufunika nywele zako ili kufanya joto lisipenye ziache kwa dk 30,Kisha zisuuze kwa maji Safi,Kisha zichane kwa taratibu ,Kisha paka mafuta ya maji kama mafuta ya Nazi ama olive oil haushauriwi kutumia mafuta ya mgando kwasababu yanaleta mba.

4. Yai

Yai hutumiwa sana na watu wengi duniani. Yai lina protini nyingi ambayo hutumika katika mfumo mpya wanywele.Tambua kuwa maji ya yai Yana madini ya sulphur,zinc,iron,selenium,phosphorous na iodine.

Jinsi ya kuandaa

Chukua yai lako moja toboa kidogo toa maji yake tu bila kiini cha njano,Kisha weka kwenye bakuli safi,Kisha weka Kijiko kimoja cha olive oil(mafuta ya mzeituni) ,Kisha Kijiko kimoja cha asali changanya kwa pamoja, Kisha paka kwenye scalp acha kwa dakika 20 then zioshe kwa shampuu.

Tumia njia hizo kuutengeneza urembo wako Mimi nimeona matokeo mazuri wewe je.